• HABARI MPYA

  Wednesday, November 15, 2017

  MBEYA CITY WANACHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA COASTAL UNION TANGA LEO

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  TIMU ya Mbeya City jioni ya leo inacheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Meneja wa Mbeya City, Geoffrey Katepa amesema kwamba katika kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wameamau kuweka kambi Tanga ambako walifika jana.
  Katepa amesema kwamba watacheza mechi leo jioni Uwanja wa Mkwakwani na baada ya hapo wataendelea na mazoezi hadi Ijumaa watakapoondoka kwenda Dar es Salaam.
  Mbeya City watakuwa wageni wa Yanga Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam Jumapili.
  Na Katepa amesema baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, wakifungwa 1-0 na zote Azam Dar es Salaam na Simba mjini Mbeya, hawataki kupoteza mechi ya Jumapili.
  “Haitakuwa vizuri tukipoteza na mechi ya Jumapili pia, kwa sababu itakuwa mechi ya tatu mfululizo, ndiyo maana tumeweka program nzuri ya maandalizi tufanye vizuri kwenye mchezo wetu ujao,”amesema Katepa ambaye ni kiungo wa zamani wa Yanga. 
  Kwa ujumla baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kirafiki za kimataifa zikiwemo za kufuzu Kombe la Dunia, Ligi Kuu inatarajiwa kurejea wikiendi hii na Ijumaa Singida United wataikaribisha Lipuli ya Iringa Uwanja wa Namfua, wakati Azam FC watakuwa wageni wa Njombe Mji FC Jumamosi Uwanja wa Saba Saba.
  Mechi nyingine za Jumamosi, Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Stand United n Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Maji Maji na Mbao FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea na Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WANACHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA COASTAL UNION TANGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top