• HABARI MPYA

  Friday, November 17, 2017

  JOSHUA AGONGESHA MWAMBA KWA SHUTI ZURI MBELE YA CANNAVARO

  BINGWA wa dunia wa ngumi za kulipwa, Anthony Joshua ameonyesha umahiri wake na mkwenye soka baada ya kupiga shuti la mbali na kugongesha mwamba.
  Joshua alionyesha ujuzi wake baada ya kupiga shuti la mguu wa kulia katika shindano la kugongesha mwamba.
  Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akifanya hayo pamoja na beki wa zamani wa Real Madrid na Juventus, Fabio Cannavaro.
  Joshua ameposti video kwenye instagram kuonyesha ujuzi wake wa soka akiambatanisha na maelezo: "Shindano la kugongesha mwamba. Ningeweza kucheza soka! Ngumi ziliniteka zaidi..."

  Anthony Joshua (kushoto) akiwa na beki wa zamani wa wa Real Madrid na Juventus, Fabio Cannavaro PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Pia ameposti picha yake akiwa amesimama na Cannavaro, aliyekuwa Nahodha wa Italia ikitwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 Ujerumani.
  Joshua ameandika maelezo kwenye picha hiyo yasemayo: "Vizuri kuwa na @fabiocannavaoofficial katika soka jioni hii'.
  Baada ya kucheza soka, Joshua akahamia kwenye mchezo mwingine na akaposti picha anacheza tenisi.
  Baada ya kustaafu soka mwaka 2011, Cannavaro amekuwa kocha na sasa akiwa ana umri wa miaka 44 anafundisha Guangzhou Evergrande, baada ya kutwaa taji la Ligi Daraja la Kwanza China na klabu ya Tianjin Quanjian mwaka jana.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA AGONGESHA MWAMBA KWA SHUTI ZURI MBELE YA CANNAVARO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top