• HABARI MPYA

  Monday, November 20, 2017

  DIDIER DROGBA KUSTAAFU SOKA NOVEMBA MWAKA 2018

  MWANASOKA bora wa zamani Afrika, Didier Drogba atastaafu soka baada ya msimu wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Marekani Novemba mwaka 2018.
  Muivory Coast huyo aliyeshinda mataji manne ya Ligi Kuu ya England akiwa na Chelsea, kwa sasa anachezea Phoenix Rising inayoshiriki ligi ya pili kwa ukubwa Marekani.
  Kwa ujumla, Drogba mwenye umri wa miaka 39 sasa, alishinda mataji 14 na Chelsea katika kipindi chake chote akicheza zaidi ya mechi 380.
  "Ah, unataka habari ya peke yako? Nafikiri mwakani utakuwa msimu wangu wa mwisho,"alisema Drogba RMC Sport ya Ufaransa. 
  Didier Drogba amesema atastaafu soka baada ya msimu wa Ligi Daraja la Kwanza nchini Marekani Novemba mwaka 2018

  "Inafikia mahali unatakiwa kuacha. Nahitaji kupata muda wa kushughulikia miradi yangu mingine. Ni vizuri kucheza, lakini kwa miaka 39, inatosha," amesema.
  Drogba amecheza zaidi ya mechi 670 katika klabu mbalimbali alizopitia ikiwemo Olympique Marseilleya Ufaransa na Galatasaray ya Uturuki.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIDIER DROGBA KUSTAAFU SOKA NOVEMBA MWAKA 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top