• HABARI MPYA

  Saturday, November 11, 2017

  AZAM FC YAICHAPA 2-0 KILIMANJARO WARRIORS CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imeichapa timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23, Kilimanjaro Warriors mabao 2-0, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika asubuhi ya leo Uwanja wa nyasi za kawaida Azam Complex, Dar es Salaam.
  Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote mbili, ulikuwa ni mahususi kwa ajili ya kikosi cha Azam FC kujiweka kwenye ushindani ikiwemo maandalizi kuelekea mtanange ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Njombe Mji utakaofanyika Novemba 18 mwaka huu.
  Enock Atta Agyei amefunga bao la pili kwa mpira wa adhabu Azam ikishinda 2-0 dhidi ya Kilimanjaro Warriors 

  Mabao ya Azam FC yalifungwa na nahodha msaidizi Aggrey Moris, dakika ya 41 aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na winga Enock Atta Agyei, faulo hiyo iliyotokana na Ramadhan Singano, kufanyiwa madhambi.
  Winga Joseph Mahundi aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Agyei, aliipatia Azam FC bao la pili dakika ya 48 akimalizia kwa mguu wake krosi safi aliyopenyezewa na beki wa kushoto Bruce Kangwa.
  Katika mchezo huo, Kocha Mkuu Aristica Cioaba, aliweza kuwatumia wachezaji wake wote kikosini waliokuwa fiti.
  Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kitapumzika kesho Jumapili kabla ya kurejea mazoezini keshokutwa Jumatatu, kuendelea na maandalizi ya kuivaa Njombe Mji, mchezo utakofanyika Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA 2-0 KILIMANJARO WARRIORS CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top