• HABARI MPYA

  Friday, November 17, 2017

  AMR FAHMY AVAA VIATU VYA BABA YAKE CAF, AWA KATIBU MKUU

  MTOTO wa Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) amekuwa Katibu Mkuu mpya wa bodi hiyo ya mpora wa miguu barani.
  Mmisri, Amr Fahmy ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CAF, nafasi ambayo baba yake Mostafa Fahmy aliitumikia kwa miaka 28. 
  Amr anachukua nafasi ya Hicham El Amrani wa Morocco ambaye alikaa kwenye nafasi hiyo tangu Oktoba mwaka 2010 hadi Machi 2017 alipojiuzulu bila sababu. 
  Fahmy ni pendekezo la Rais wa CAF, Ahmad kwa Kamati ya Utendaji ambayo imeidhinisha uteuzi wake katika kikao chake cha jana mjini Rabat, Morocco.
  Amr Fahmy ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CAF, nafasi ambayo baba yake Mostafa Fahmy aliitumikia kwa miaka 28 

  Makatibu wawili wasaidizi pia wameteuliwa kwa vigezo vile vile, wa kwanza ni Mghana Anthony Baffoe ambaye anakuwa Msaidizi upande wa Maendeleo na Mashindano na wa pili ni Mmorocco, Essadik Alaoui anayekuwa Msaidizi upande wa Utawala na Fedha.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMR FAHMY AVAA VIATU VYA BABA YAKE CAF, AWA KATIBU MKUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top