• HABARI MPYA

  Wednesday, October 18, 2017

  YANGA WASHINDWA KUIFUNGA RHINO RANGERS, SARE 0-0 MWINYI

  Na Adam Hhando, TABORA
  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wametoka sare ya bila kufungana na wenyeji, Rhino Rangers katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Kocha Mzambia, George Lwandamina alianzisha wachezaji wengi ambao siku za karibuni wamekuwa hawana nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
  Rhino ilichezesha kikosi chake kamili cha kwanza na ikatoa upinzani wa kutosha kwa Yanga, ambao walikuwa wanacheza hapa kwa mara ya kwanza tangu Oktoba 31 mwaka 2015 walipomenyana na Kagera Sugar katika Ligi Kuu, wakati huo ikitumia Uwanja huh kupisha ukarabati kwenye Uwanja wao wa Kaitaba, Bukoba.
  Gardiel Michael, Ibrahim Hajib, Geoffrey Mwashiuya na Papy Tshishimbi wote walingia kipindi cha pili leo

  Kipindi cha pili, timu zote zilifanya mabadiliko na dakika za 10 za mwisho Lwandamina akaingiza ‘majembe’ yake akina Gardiel Michael, Papy Kabamba Tshishimbi, Ibrahim Hajib, Geoffrey Mwashiuya na wengineo ambao walikwenda kuuchangamsha zaidi mchezo.
  Lakini ngome ya Rhino Rangers ilisimama imara kuwadhibiti nyota hao wa Yanga wasilete madhara upande wake.
  Baada ya mchezo huo, Ijumaa Yanga itaondoka mjini hapa kwenda Shinyanga ambako Jumapili watamenyana na wenyeji, Stand United katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Kikosi cha Rhino Rangers kilikuwa; Mohammad Seif, Ally Mwanyiro/Juma Amani dk67, Petro Joseph, Joseph Mnyango, Jamal Juamanne/Yussuf Mputa dk81, Julius Elius/Shani Shiraz dk56, Ibrahim Bona/Athumani Matata dk74, Sameer Mwinshehe, Edger Mwaiponja/Hamza Juma dk64, Adam Kindemba na Ramadhan Mwinyimbegu.
  Yanga SC; Benno Kakolanya/Ramadhani Kabwili dk83, Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali/Gardiel Michael dk65, Andrew Vincent ‘Dante’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Abdallah Hajji ‘Ninja’ dk65, Said Juma ‘Makapu’/Papy Kabamba Tshishimbi dk83 , Baruan Akilimali/Mussa Said dk65, Maka Edward, Matheo Anthony/Ibrahim Hajib dk83, Yussuf Mhilu/Juma Mahadhi dk65 na Emmanuel Martin/Geoffrey Mwashiuya dk83.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WASHINDWA KUIFUNGA RHINO RANGERS, SARE 0-0 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top