• HABARI MPYA

    Saturday, October 21, 2017

    SIMBA NA MJI NJOMBE 'WAFANYIANA' WAKIGOMBEA MLANGO UHURU

    Askari Polisi wakiwadhibiti 'makomandoo' wa timu za Simba na Njombe Mji FC kwenye mlango wa kuingilia Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakigombea kila upande uanze kuingiza wachezaji wake ndani kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoanza Saa 10:00 jioni ya leo
    Askari Polisi wakimdhibiti kiongozi wa Simba, Hamisi Kisiwa
    Vurugu getini, kulia ni makomandoo wa Njombe Mji na kushoto wa Simba
    Madereva wa gari zote mbili, la Simba (kushoto) na Njombe (kulia) walizikutanisha katika kugombea kuanza kushusha wachezaji waingie ndani
    Askari wakiwasukuma nyuma makomandoo wa Njombe Mji ili wachezaji wa Simba wapite kwanza
    Haikuwa kazi rahisi kutokana na ubishi wa makomandoo wa Njombe
    Hata hivyo, Simba walifanikiwa kuingiza wachezaji wao kwanza na mlango ukafungwa ili waondoke na Njombe nao wasogee 
    Gari la Simba linarudi nyuma baada ya kushusha wachezaji
    Gari la Njombe Mji linasogea kushusha wachezaji wake
    Basi la Simba likiwa limepaki baada ya kushusha wachezaji 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA MJI NJOMBE 'WAFANYIANA' WAKIGOMBEA MLANGO UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top