• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2017

  SAFARI YA OZIL KWENDA MAN UNITED YAZIDI KUKARIBIA

  KIUNGO Mesut Ozil anamtaka Jose Mourinho amuokoea kutoka kwenye matatizo ya Arsenal  na ameuandaa moyo wake kujiunga na Manchester United mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.
  Inadaiwa Ozil amewaambia rafiki zake kwamba anaamini Mourinho atamchukua msimu ujao kama hayatabadilika katika miezi hii
  Ozil atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu baada ya kuwaambia Arsenal hayuko tayari kusaini mkataba mpya.
  Arsenal inatazamiwa kuondoa uwezekano wa kumpoteza Ozil kwenda United bure msimu ujao kwa kumtafuta mnunuzi wa mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani dirisha la usajili litakapofunguliwa tena mwezi Januari.
  Mesut Ozil anataka Jose Mourinho amnunue Manchester United kumuokoa na matatizo ya Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Timu chache tu zinamuhitaji Ozil, lakini Arsenal inajiamini itampata mnunuzi kabla ya mkataba wake kumalizika.
  Inter Milan imeonyesha nia ya kumsajili Ozil kwa kuzungumza hadharani, lakini nyota huyo wa zamani wa Real Madrid anaamini United watamchukua Januari.
  Ozil na Mourinho wana historia ndefu ya mahusiano baada ya awali kufanya kazi pamoja Bernabeu. Na hata baada ya wawili hao kuachana Hispania, Mourinho aliendelea kumthaminisha Ozil kama mmoja wa viungo wabunifu duniani.
  Licha ya kipaji chake cha kuzaliwa nacho, lakini Ozil ameshindwa kufanya vizuri kuonyesha thamani yake ya kusajiliwa Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 42.5 mwaka 2013.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAFARI YA OZIL KWENDA MAN UNITED YAZIDI KUKARIBIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top