• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2017

  RHINO RANGERS WAWAFUATA TOTO NA PAMBA KIBABE MWANZA

  Na Adam Hhando, TABORA
  KIKOSI cha Rhino Rangers cha hapa Tabora kimeondoka jioni hii kwenda mjini Mwanza kucheza mechi zao mbili za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara dhidi ya Toto Africans na Pamba.
  Maafande hao maarufu kwa jina la Faru Weusi, wanaenda Jijini Mwanza wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare mechi mbili mfululizo dhidi ya Biashara ya Mara katika Ligi na dhidi ya Yanga katika mechi ya kirafiki Jumatano zote zikichezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Katibu mkuu wa Rhino Rangers, Dickson Mgalike amesema timu imeondoka na wachezaji 23 pamoja na viongozi wanane, huku ikitarajiwa kurudi Tabora baada ya mchezo dhidi ya Pamba Oktoba 28 kufuatia kucheza na Toto Africans Jumapili.
  Rhino Rangers imewahi kucheza Ligi Kuu msimu wa 2013-2014 
  Mgalike amesema wachezaji wote wako vizuri isipokuwa wale majerahu kwa muda mrefu ambao ni kiungo mshambuliaji Hussein Abdallah  ‘Cheppe’ na mshambuliaji Juma Shekha.
  Ikumbukwe kuwa hizo zitakuwa mechi za mwisho katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Kwanza kwa upande wa Rhino, kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili katikati ya mwezi Novemba.
  Rhino ipo Kundi C na inashika nafasi ya sita kwa pointi zake tano, ikiziwa pointi saba na vinara Dodoma FC ya kocha Jamhuri Kihwelo walio mbele ya Alliance ya Mwanza yenye pointi 10, Transit Campo ya Dar es Salaam pointi saba, JKT Oljoro pointi sita, Toto Africans na Biashara wenye pointi tano kila moja 5, wakati Pamba inaburuza mkia kwa pointi zake tatu. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RHINO RANGERS WAWAFUATA TOTO NA PAMBA KIBABE MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top