• HABARI MPYA

  Monday, October 16, 2017

  MSUVA ASETI BAO LA KWANZA DIFAA YASHINDA 2-0 MOROCCO NA KUSONGA MBELE LA LIGI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana ameseti bao la kwanza, timu yake Difaa Hassan El Jadida ikishinda 2-0 katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Ligi Morocco dhidi ya Chabab Rif Hoceima Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida.
  Msuva alitia krosi maridadi dakika ya 64 ikatua kichwani kwa Adnane El Ouardy akaudondoshea mpira nyavuni kuipatia bao la kwanza Jadida, kabla ya Hamid Ahadad kufunga la pili dakika ya 89.
  Simon Msuva (katikati) walioinama katika kikosi cha Difaa Hassan El Jadida kilichoanza jana


  Kwa matokeo hayo, Jadida inatinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2, baada ya wiki iliyopita kufungwa 2-1 Uwanja wa Mimoun Al Arsi mjini Al Hoceima, siku ambayo Msuva aliifungia timu yake bao muhimu la ugenini.
  Katika mchezo wa jana, Msuva alipumzishwa dakika ya 92 na nafasi yake kuchukuliwa na Tarik Astati.
  Baada ya mchezo huo, Difaa ambayo ina viporo viwili dhidi ya FUS Rabat na Wydad Cassablanca, itamenyana na FAR Rabat Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA ASETI BAO LA KWANZA DIFAA YASHINDA 2-0 MOROCCO NA KUSONGA MBELE LA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top