• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2017

  MSUVA AISAIDIA DIFAA KUWAZIMA FAR RABAT KWAO LIGI YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, RABAT
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku huu ameisaidia timu yake, Difaa Hassan El-Jadida kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola dhidi ya wenyeji FAR Rabat Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat.
  Katika mchezo wa leo, Msuva alianzia benchi na baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana, Difaa wakafanya mabadiliko.
  Na miongoni mwa wachezaji walioingia ni winga wa zamani wa Yanga, Simon Happygod Msuva, mfungaji bora mara mbili na mchezaji bora mara moja wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Simon Msuva (kushoto) akifurahia na wachezaji wenzake baada ya kuisaidia Difaa Hassan El-Jadida kushinda 2-1 ugeninidhidi ya wenyeji FAR Rabat
  Hata hivyo, ni wenyeji FAR Rabat waliotangulia kupata bao kupitia kwa kiungo Mohamed El Fakih dakika ya 52, kabla ya Bilal Al-Makri kuisawazishia DHJ dakika ya 55.
  Shujaa wa Difaa Hassan El- Jadida leo ni Hamid El Ahadad aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 na ushei na kuwanyamazisha mashabiki wa timu wenyeji.
  Ilikuwa ni furaha kubwa kwa Msuva na wachezaji wenzake baada ya mechi hiyo kutokana na ushindi huo wa ugenini dhidi ya moja ya timu tishio Morocco na Kaskazini mwa Afrika kwa ujumla.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AISAIDIA DIFAA KUWAZIMA FAR RABAT KWAO LIGI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top