• HABARI MPYA

    Sunday, October 15, 2017

    MOROCCO WAPEWA UENYEJI CHAN, MISRI NAO KUSHIRIKI

    MOROCCO ndio wenyeji wapya wa fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
    Hiyo inafuatia kikao cha Kamati ya Dharula ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kilichofanyika jana mjini Lagos, Nigeria chini ya Uenyekiti wa Rais wa CAF Ahmad kuipa jukumu hilo Shirikisho la Soka Moroccan (RMFF).
    KIkao hicho kilifanyika ili kupata nchi mbadala ya kuandaa mashindano hayo mapema mwakani, kufuatia kujitoa kwa Kenya.
    Nchi nyingine iliyoomba kuipokea Kenya ni Equatorial Guinea, wakati Ethiopia pamoja na kuonyesha nia lakini haikuwasilisha barua ya kuungwa mkono na Serikali yao, ambayo ni lazima kwa mujibu wa sheria za CAF za kuomba yenyeji wa michuano yake.
    Sasa Fainali za Total CHAN nchini Morocco 2018 zinatarajiwa kuanza Januari 12 hadi Februari 4 mwakani, zikishirikisha timu 16 zenye wachezaji ambao wanacheza nchini mwao tu.
    Na kufuatia Morocco kupewa uenyeji wa CHAN 2018, Kamati ya Dharula ua CAF imeipitisha Misri kushiriki fainali hizo. 
    Katika mechi za mchujo kwa Kanda ya Kaskazini, Misri ilitolewa na Morocco ambao kwa kuwa wenyeji sasa wanashiriki moja kwa moja bila kigezo cha kufuzu na Mafarao sasa ndiyo wataiwakilisha kanda hiyo.
    Hizi zitakuwa fainali za kwanza za Misri tangu waliposhiriki fainali za kwanza kabisa za CHAN mwaka 2009.
    Wakati huo huo, Kamati ya Dharula ya CAF imetupilia mbali pingamizi la Mali na kuithibitisha Mauritania kushiriki Total CHAN kwa mara ya pili, baada ya mwaka 2014 nchini Afrika Kusini.
    Nchi 16 zitakazoshiriki Total CHAN Morocco 2018 ni Misri, Libya na Morocco Kanda ya Kaskazini, Ethiopia na Uganda Kanda ya Mashariki na Kati, Cameroon, Kongo na Equatorial Guinea Kanda ya Kati, Guinea na Mauritania Magharibi A, Burkina Faso, Ivory Coast na Nigeria Magharibi B, Angola, Namibia na Zambia Kanda ya Kusini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOROCCO WAPEWA UENYEJI CHAN, MISRI NAO KUSHIRIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top