• HABARI MPYA

  Thursday, October 19, 2017

  MESSI AFIKISHA MABAO 100 ULAYA BARCA IKISHINDA 3-1

  Lionel Messi akifumua shuti kuifungia Barcelona kufikisha mabao 100 kwenye michuano ya Ulaya jana Uwanja wa Camo Nou PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  MABAO YA MESSI ULAYA

  97 Ligi ya Mabingwa
  3   Super Cup 
  11 Penalti
  82 Mguu wa kushoto
  14 Mguu wa kulia 
  4   Kichwa 
  16 Kutoka nje ya boksi 
  5   Mipira ya adhabu ya moja kwa moja 
  MSHAMBULIAJI Muargentina, Lionel Messi jana amefikisha mabao 100 katika michuano ya klabu Ulaya.
  Hiyo ni baada ya Messi jana kuifungia bao la pili Barcelona dakika ya 61 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Olympiacos kwenye mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Camp Nou, mabao mengine ya Barca yamefungwa na Dimitrios Nikolaou aliyejifunga dakika ya 18 na Lucas Digne dakika ya 64. 
  Nikolaou akaifungia bao la kufutia achozi Olympiacos dakika ya 89.
  Mapema dakika ya 42, refa Mscotland, William Collum alimtoa kwa kadi nyekundu beki, Gerard Pique baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AFIKISHA MABAO 100 ULAYA BARCA IKISHINDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top