• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2017

  MBAO FC YAPANIA KUWAFUNGA AZAM KESHO WAWAPOZE MASHABIKI WAO

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi amesema kwamba lazima washinde dhidi ya Azam FC kesho ili kurejesha imani ya mashabiki wa timu hiyo.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online juzi mjini Dar es Salaam, Njashi alisema kwamba hali si nzuri baada ya timu kucheza mechi tano mfululizo bila ushindi.
  “Tunafahamu utakuwa ni mchezo mgumu, lakini lazima tupambane tushinde, kwa sababu hali si nzuri kwa sasa, tumecheza mechi tano bila kushinda,”alisema Njashi.
  Mwenyekiti wa timu ya Mbao FC ya Mwanza, Solly Zephania Njashi (kushoto) 

  Baada ya ushindi wa 1-0 ugenini Agosti 26 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Mbao ikaenda kufungwa mechi mbili nyingine za ugenini na kutoa sare tatu mfululizo nyumbani.
  Ilifungwa 2-1 mara mbili, kwanza na Singida United Septemba 10 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na baadaye na Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro Septemba 16. 
  Mechi nyingine tatu za nyumbani Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Mbao ilitoa sare ya 2-2 na Simba SC Septemba 21, 1-1 na Tanzania Prisons Septemba 30 na 2-2- tena na Mbeya City Oktoba 13.
  Baada ya mchezo dhidi ya Azam FC kesho, Mbao watatoka tena kwa mechi tatu za ugenini Nyanda za Juu Kusini dhidi ya Lipuli, Njombe Mji na Maji Maji kuanzia Oktoba 27.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBAO FC YAPANIA KUWAFUNGA AZAM KESHO WAWAPOZE MASHABIKI WAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top