• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2017

  MAN UNITED WAPATA PAUNI MILIONI 40 KWA KUBEBA KOMBE LA ULAYA

  Manchester United imepata Pauni Milioni 40 kwa kutwaa Kombe la Europa League mwezi Mei mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  MCHANGANUO WA MALIPO YA MAN UNITED (KATIKA EURO)

  Posho ya ushiriki:  2,600,000
  Posho ya Uchezaji: 1,904,000 
  Masoko: 29,649,170
  Hatua ya 32 Bora: 500,000
  Hatua ya 16 Bora: 750,000
  Robo Fainali: 1,000,000
  Nusu Fainali: 1,600,000
  Fainali: 6,500,000
  Jumla: 44,503,170 (Pauni Milioni 40)
  TIMU ya Manchester United imepata kiasi cha Pauni Milioni 40 kwa kutwaa Kombe la Europa League msimu uliopita na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. 
  Kikosi cha Jose Mourinho, kimepatiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kuliko wapinzani wao kutokana na mgawanyo wa fedha za haki ya matangazo ya Televisheni nchini England. 
  Mechi zote za United za Europa League zilionyeshwa na Televisheni ya BT Sport ambao waliongeza ada za mwisho.
  Wana fainali wenzao, Ajax ambao walifungwa 2-0 kwenye fainali kwa mabao ya Paul Pogba na Henrikh Mkhitaryan, walipewa Pauni Milioni 14 licha ya kucheza mechi sawa na Man United.
  Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya pia, Juventus waliofungwa kwenye fainali waliongoza kwa kupata fedha baada ya kupewa Pauni Milioni 99 na UEFA msimu uliopita.
  Leicester City waliwazidi mabingwa, Real Madrid kwa kushika nafasi ya pili kwa sababu mabingwa hao wa wakati huo wa England walipata fedha zaidi za haki ya matangazo ya TV.
  Mikataba ya haki za matangazo ya Televisheni Uingereza na Italia ilikuwa ma thamani zaidi na ziligawana klabu chache tofauti na Hispania, tano.
  Leicester walipata Pauni Milioni 73.2 kutoka UEFA na Madrid walipata Pauni Milioni 72.6.
  Klabu nyingine za England, Arsenal ilipata Pauni Milioni 58, Manchester City Pauni Milioni 45 na Tottenham Pauni Milioni 39 kwa ushiriki wao Ligi ya Mabingwa. 
  Katika timu 32 za makundi, Basel ndio waliopata kidogo zaidi, Pauni Milioni 14.6 katika karibu Pauni Bilioni 1.25 za zawadi za UEFA.

  ZAWADI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA

  Juventus: Pauni Milioni 99
  Leicester: Pauni Milioni 73.2
  Real Madrid: Pauni Milioni 72.6
  Napoli: Pauni Milioni 59
  Monaco: Pauni Milioni 58 
  Arsenal: Pauni Milioni 58
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WAPATA PAUNI MILIONI 40 KWA KUBEBA KOMBE LA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top