• HABARI MPYA

  Thursday, October 19, 2017

  MADJER AREJESHWA KUFUNDISHA ALGERIA BAADA YA MATOKEO MABAYA

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa FC Porto, Rabah Madjer ameteuliwa kuwa kocha wa Algeria kwa mara ya nne.
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 anachukua nafasi ya Mspaniola, Lucas Alcaraz, ambaye amefukuzwa baada ya matokeo mabaya kwenye mechi za kufuzu Kome la Dunia.
  Algeria imevuna pointi moja tu kutoka kwenye mechi zao tano kwenye Raundi ya Tatu, na Madjer – aliyeifungia mabao 28 nchi yake katika mechi 87 – anapewa timu kuelekea mechi yao ya mwisho ya Kundi B dhidi ya Nigeria mwezi ujao.
  Rabah Madjer ameteuliwa kuwa kocha wa Algeria kwa mara ya nne

  Madjer, ambaye mara ya mwisho aliifundisha timu hiyo mwaka 2002, anakumbukuzwa zaidi kwa bao lake la kusawazisa kwenye fainali ya Kombe la Ulaya mwaka 1987 ambayo Porto walishinda 2-1 dhidi ya Bayern Munich.
  Madjer, mwenye umri wa miaka 58, anakuwa kocha wa tano wa timu ya taifa ndani ya miaka mitatu na anachukuliwa wakati timu imekwishatolewa kwenye mbio za kufuzu Kombe la Dunia 2018.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MADJER AREJESHWA KUFUNDISHA ALGERIA BAADA YA MATOKEO MABAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top