• HABARI MPYA

  Thursday, October 19, 2017

  KYLIAN MPABBE ALIVYOVUNJA REKODI YA KLUIVERT LIGI YA MABINGWA

  Kylian Mbappe akishangilia baada ya kufunga bao lake la nane kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

   WAFUNGAJI BORA  VIJANA KATIKA  HISTORIA  YA LIGI YA  MABINGWA  ULAYA
  MCHEZAJIMABAO
  Kylian Mbappe (Monaco, PSG)8
  Patrick Kluivert (Ajax)7
  Karim Benzema (Lyon)6
  Raul (Real Madrid)6
  Bojan Krkic (Barcelona)5
  Yakubu (Maccabi Haifa)5
  Obafemi Martins (Inter Milan)4
  Miralem Pjanic (Lyon)4
  Alan Dzagoev (CSKA Moscow)3
  Goncalo Guedes (Benfica)3
  Marquinhos (Roma, PSG)3
  Arjen Robben (PSV)3
  Wayne Rooney (Manchester United)3
  Tomas Rosicky (Sparta Prague)3
  Javier Saviola (Barcelona)3
  Theo Walcott (Arsenal)3
  MFARANSA Kylian Mbappe ameendelea kuvuna rekodi katika ulimwengu wa soka.
  Jana usiku, mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain amekuwa mfungaji wa mabao mengi kijana kihistoria kiwango kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, akifikisha mabao manane baada ya mechi 12 tu.
  Hiyo ni baada ya chipukizi huyo kufunga bao moja katika ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Anderlecht kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Constant Vanden Stock mjini Brussel, Ubelgiji. Mbappe alifunga dakika ya tatu na mabao mengine yakafungwa na Neymar Junior dakika ya 66, Angel Di Maria dakika ya 88 na Edinson Cavani dakika ya 44.
  Hilo lilikuwa bao lake la pili katika Ligi ya Mabingwa msimu huu, ambayo yanajumuishwa na sita aliyofunga akiwa na Monaco wakifika Nusu Fainali msimu uliopita.
  Bao hilo linamfanya ampiku Patrick Kluivert ambaye alikuwa anashikiliwa rekodi ya kufunga mabao mengi akiwa ana umri wa miaka 21.
  Mshambuliaji huyo wa Uholanzi, alifunga mabao saba kwenye ndani ya misimu miwili kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na Ajax kabla ya kusherehekea miaka 20 ya kuzaliwa kwake, likiwemo bao maarufu la ushindi dhidi ya AC Milan kwenye fainali mwaka 1995.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KYLIAN MPABBE ALIVYOVUNJA REKODI YA KLUIVERT LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top