• HABARI MPYA

  Thursday, October 19, 2017

  KIPA WA BENFICA AVUNJA REKODI YA CASILLAS KWA MACHUNGU

  MMOJA baada ya mwingine alikwenda kumkumbatia Mile Svilar ambaye machozi yalikuwa yanamlenga mwishoni mwa mchezo. 
  Wachezaji katika jezi zote, nyekundu na nyeusi walimfuata kipa kinda namba moja wa Benfica kumpa maneno ya kumfariji.
  Mlinda mlango huyo mdogo zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alijua mechi yake ya kwanza Ulaya itakuwa ya kukumbukwa kwa kuwapa ushindi Manchester United.
  Ni mechi ambayo imekiweka kikosi cha Jose Mourinho katika nafasi nzuri ya kwenda hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuendeleza rekodi yao ya ushindi kwa asilimia 100 kwenye Kundi A, huku ikikata matumaini ya Benfica kusonga mbele. 
  Ushindi mwingine katika mchezo mwingine utakaozikutanisha timu hizo Uwanja wa Old Trafford utathibitisha hilo. 
  Svilar atajutia kosa lake alilolifanya dakika ya 64 ambalo liliisaidia United kupata bao pekee la ushindi.

  Svilar akilalamika huku ameshika mpira kupinga bao la Manchester United PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Marcus Rashford alipiga mpira wa adhabu katikati kutoka kwenye nusu ya eneo la Benfica, lakini haikufahamika kama Svilar alikuwa amekaa vibaya. 
  Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 na siku 52, ni mdogo zaidi ya Iker Casillas wakati anadaka kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo na jana alikuwa mbele kidogo kwa hatua moja kutoka kwenye mstari wa lango.
  Hivyo ilikuwa rahisi kufungwa kwa shuti la mbali la mpira wa adhabu, japo alijitahidi kurudi nyuma na kuokoa mpira akiwa ndani kabisa ya lango lake bila kujua kwamba teknolojia ya kwenye mstari wa lango ingemuumbua.
  Kocha Mourinho alimsifu kipa huyo ni mzuri na kosa alilolifanya hufanywa hata na makipa wakubwa pia na kuruhusu mabao rahisi ya aina hiyo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA WA BENFICA AVUNJA REKODI YA CASILLAS KWA MACHUNGU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top