• HABARI MPYA

  Tuesday, October 17, 2017

  JOSHUA ABADILISHIWA MPINZANI BAADA YA MBLUGARIA KUUMIA BEGA

  PAMBANO la Anthony Joshua na Kubrat Pulev limeahirishwa baada ya Mbulgaria kuumia mazoezini na sasa nafasi yake itachukuliwa na Carlos Takam.
  Pulev alitarajiwa kupambana na bingwa wa mataji ya IBF na WBA, Joshua Oktoba 28, mwaka huu Uwanja wa Principality mjini Cardiff, Uingereza, lakini maumivu ya bega yamevuruga mpango huo.
  Mfaransa Takam, ambaye mshindani namba tatu wa IBF, Jumatatu alikamilisha dili la kuchukua nafasi hiyo dakika za mwishoni kama mpinzani asiyejulikana, mwenye umri wa miaka 36 ambaye amepoteza mapambano matatu kati ya 39 aliyopigana.

  Anthony Joshua sasa atapigana na Mfaransa Carlos Takam baada ya Mbulgaria Kubrat Pulev kuumia bega na kujitoa PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Promota wa Joshua, Eddie Hearn amesema: "Nimepokea simu mchana kabisa kuambiwa kwamba Pulev ameumia bega lake na anaweza kujitoa kwenye pambano – ambayo baadaye ikathibitishwa na Daktari wake. Sheria za IBF zinasema nafasi hiyo atapewa mpiganaji mwingine kwenye mstari, ambaye ni Carlos Takam.
  "Wakati pambano la Pulev linatangazwa, nilikubaliana na timu ya Takam waanze kambi na kujiweka tayari kwa pambano hili. Nilipowapigia jioni hii walikuwa wenye furaha kupita kiasi na waklio tayari kwenda.
  "Ni ngumu kwa AJ aliyejitayarisha kupigana na Pulev kulingana na anavyomjua, sasa anakutana na mtu tofauti kabisa mwenye aina nyingine ya upiganaji, Takam – hii haijawahi kutokea kwake tangu ameanza mchezo huu, lakini yuko tayari kwa wote watakaokuja Oktoba 28,".
  Pulev anakuwa bondia wa pili kujitoa kwenye pambano na Joshua, baada ya awali Wladimir Klitschko mtu wa kwanza halisi aliyepangwa kwenye pambabo hili ambalo lingekuwa la marudiano baada ya kupigwa Aprili kuamua kustaafu kabisa masumbwi.
  Lakini tayari zaidi ya tiketi 70,000 zimeuzwa katika pambano lake la 20 la ngumi za kulipwa. Umati wa watu 80,000 unatarajiwa kuwapo uwanjani siku hiyo, maana yake pambano hilo litavunja rekodi ya dunia ya kuhudhuriwa na watu wengi, tangu mwaka 1978 Muhammad Ali alipopigana Leon Spinks mbele ya watu 63,315 New Orleans Superdome.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA ABADILISHIWA MPINZANI BAADA YA MBLUGARIA KUUMIA BEGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top