• HABARI MPYA

    Thursday, October 19, 2017

    HALI HALISI JENGO LA YANGA NA UWANJA WA KAUNDA KWA SASA

    Mwonekano wa jengo la makao makuu ya klabu ya Yanga, upande wa Uwanja wa Kaunda liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam ulivyoathiriwa na kufurika kwa madimbwi ya maji katika eneo la Jangwani
    Angalau mwonekano wa jengo unakuwa wa kuvutia kidogo unapopanda juu, ingawa kupauka kwa rangi na kuchakaa kwa jengo lenyewe ni tatizo lingine
    Mandhari ya jengo la klabu hiyo inapoteza mvuto wake kila kukicha tangu likarabatiwe kwa mara ya mwisho 2008
    Mbele ya jengo kuna kifusi kinalundikwa kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Kaunda uanze kutumika tena
    Uongozi umesema umedhamiria kuurudisha Uwanja wa Kaunda katika ubora wake
    Pembezoni mwa ukuta wa uzio wa Uwanja wa Kaunda kuna mfereji wa maji, ambao kama yanakuwa yanakwenda vizuri kwenye mkondo wake hayawezi kuingia ndani
    Hapa ni katikati ya Uwanja wa Kaunda, ambao kihistoria umeibua vipaji vya wanasoa wengi nyota enzi zake
    Tangu 2013 Uwanja wa Kaunda umetelekezewa kabisa na matokeo yake ndiyo haya 
    Hata jengo nalo linazidi kuchakaa kila kukicha, wakati ni mwaka 2013 tu lilikuwa katika mwonekano mzuri

    Jengo la Yanga lipo barabarani kabisa makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HALI HALISI JENGO LA YANGA NA UWANJA WA KAUNDA KWA SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top