• HABARI MPYA

  Wednesday, October 18, 2017

  GULAM WA TOC AWA MWENYEITI MPYA WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR

  Na Salum Vuai, ZANZIBAR
  BARAZA la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), limepata Mwenyekiti mpya.
  Katika uteuzi wa viongozi kwenye taasisi mbalimbali za serikali uliofanywa jana Oktoba 17, 2017 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Gulam Abdulla Rashid ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo.
  Dk. Shein amemfanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 7(2) cha sheria ya Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar namba 5 ya mwaka 2010. 

  Rais wa TOC Gulam Abdalla Rashid (kulia), sasa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar  

  Rashid ambaye pia ni Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), anapokea kijiti hicho kutoka kwa Sharifa Khamis Salim ‘Sherry’ aliyekuwa akiishikilia nafasi hiyo kwa miaka mingi.
  Mwenyekiti huyo mpya pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa iliyokuwa Idara ya Michezo Zanzibar ambayo imefutwa miaka mingi sasa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GULAM WA TOC AWA MWENYEITI MPYA WA BARAZA LA MICHEZO ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top