• HABARI MPYA

  Saturday, October 21, 2017

  WYDAD NA USM ALGER KUWANIA FAINALI LIGI YA MABINGWA LEO

  TIMU ya Wydad Athletic Club inaikaribisha USM Alger kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca kuanzia Saa 4:00 usiku.
  Wydad Casablanca watahitaji ushindi lazima ili kwenda Fainali, kwani sare yoyote ya mabao itawasaidia wageni kufuatia timu hizo kutoka sare ya bila kufungana Septemba 29, mwaka huu Uwanja wa Julai 5 mjini Algiers.
  Nusu fainali nyingine ya pili ya Ligi ya Mabingwa itazikutanisha, wenyeji Al Ahly SC na  Etoile du Sahel ya Tunisia Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri kuanzia Saa 2:00 usiku. 
  Wydad Athletic wanaikaribisha USM Alger kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa leo mjini Cassablanca

  Ahly watahitaji hata ushindi wa 1-0 ili kwenda Fainali, baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Oktoba 1 Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia.
  Siku hiyo, mabao ya Etoile du Sahel yalifungwa na Alaya Brigui dakika ya 16 na Mohamed Amine Ben Amor dakika ya 74, wakati la Ahly lilifungwa na Saleh Gomaa dakika ya 66.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WYDAD NA USM ALGER KUWANIA FAINALI LIGI YA MABINGWA LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top