• HABARI MPYA

  Tuesday, September 19, 2017

  ROONEY AZUIWA KUENDESHA GARI MIAKA MIWILI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Wayne Rooney amehukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili na kufanya kazi za kijamii kwa saa 100 kufuatia kukutwa na hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa kupita kiasi.
  Rooney alikuwa amekunywa na kuzidisha kiwango cha kilevi kwa mara tatu wakati anasimamishwa na Polisi.
  Na baada ya kukiri kosa, mwanasoka huyo bilionea jana akahukumiwa kutoendesha gari katika Mahakama ya Stockport Magistrates. 
  Pamoja na adhabu hiyo, Rooney mwenye umri wa miaak 31 pia anatarajiwa kuadhibiwa zaidi kwa kukata mshahara katika klabu yake, Everton.

  Wayne Rooney akiwasili katika Mahakama ya Stockport Magistrates kusikiliza kesi yake 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROONEY AZUIWA KUENDESHA GARI MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top