• HABARI MPYA

    Monday, September 11, 2017

    PLATEAU MABINGWA WAPYA NIGERIA, OKPOTU MFUNGAJI BORA

    TIMU ya Plateau United juzi ilitawazwa kuwa bingwa mpya wa Ligi Kuu ya Nigeria baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rangers katika siku ya kuhitimisha msimu wa 2016/2017 Uwanja wa Rwang Pam Township. 
    Kwa ushindi huo, timu hiyo inayojulikana kwa jina la utani, ‘Tin City Boys’ imemaliza msimu na pointi 66 baada ya mechi 38 huku wapinzani wao wa karibu, Mountain of Fire na Miracles (MFM) waliofungwa 2-1 ugenini na El-Kanemi Warriors ya Maiduguri wakimaliza nafasi ya pili kwa pointi zao 62.
    Mjini Jos, Chukwuemeka Umeh aliifungia bao la kuongoza Plateau United mapema tu dakika ya 26 akimtungua kipa Itodo Akor, kabla ya Benjamin Turba aliyetokea benchi kipindi cha pili mwishoni mwa mchezo.
    Hilo linakuwa taji la kwanza kabisa la Ligi Kuu ya Nigeria kwa Plateau United ambayo inaingia kwenye orodha ya timu 19 zilizotwaa ubingwa wa Nigeriaa.
    Nahodha wa Plateau United akikabidhiwa Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Nigeria juzi 
    Kocha Kennedy Boboye, nyota wa zamani wa kikosi cha Olimpiki cha Nigeria, aliyejiunga na Plateau akitokea Abia Warriors mwanzoni mwa msimu, anastahili sifa zaidi kwa kushinda taji hilo katika msimu wake wa kwanza kabisa. 
    Mbali ya tiketi ya kuiwakilisha Nigeria kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani pamoja na washindi wa pili, MFM, Plateau imezawadiwa dola za Kimarekani 137,600. 
    Mabingwa mara mbili Afrika, Enyimba, waliomaliza nafasi ya tatu, watacheza michuano ya Kombe la Shirikisho wakiungana na washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Nigeria, maarufu kama FA Cup. 
    Wakati huo huo, mshambuliaji wa Lobi Stars, Anthony Okpotu aliyefunga bao lake la 19 katika sare ya 1-1 ugenini na FC Ifeanyi Ubah amekuwa mfungaji bora, huku Shooting Stars SC (3SC); ABS ya Ilorin; Gombe United na Remo Stars, zilizoshika nafasi nne za mwisho, zote zimeshuka Daraja.
    Mshambuliaji wa Lobi Stars, Anthony Okpotu amekuwa mfungaji bora kwa mabao yake 19

    ORODHA YA MABINGWA WA NIGERIA
    •1972: Mighty Jets of Jos
    •1973: Bendel Insurance
    •1974: Rangers International FC
    •1975: Rangers International FC
    •1976: Shooting Stars Sports Club (3SC)
    •1977: Rangers International FC
    •1978: Racca Rovers
    •1979: Bendel Insurance
    •1980: Shooting Stars Sports Club (3SC)
    •1981: Rangers International FC
    •1982: Rangers International FC
    •1983: Shooting Stars Sports Club (3SC)
    •1984: Rangers International
    •1985: New Nigeria Bank
    •1986: Leventis United
    •1987: Iwuanyanwu Nationale
    •1988: Iwuanyanwu Nationale
    •1989: Iwuanyanwu Nationale
    •1990: Iwuanyanwu Nationale
    •1991: Julius Berger
    •1992: Stationery Stores
    •1993: Iwuanyanwu Nationale
    •1994: BCC Lions
    •1995: Shooting Stars Sports Club (3SC)
    • 1996: Udoji United
    •1997: Eagle Cement
    •1998: Shooting Stars Sports Club (3SC)
    •1999: Lobi Stars
    •2000: Julius Berger
    •2001: Enyimba International FC 
    •2002: Enyimba International FC 
    •2003: Enyimba International FC 
    •2004: Dolphins F.C.
    •2005: Enyimba International FC 
    •2006: Ocean Boys FC
    •2007: Enyimba International FC 
    •2008: Kano Pillars F.C.
    •2009: Bayelsa United
    •2010: Enyimba International FC 
    •2011: Dolphins F.C.
    •2013: Kano Pillars F.C.   
    •2014: Kano Pillars F.C.   
    •2015: Enyimba International FC 
    •2016: Rangers International FC
    •2017: Plateau United FC
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLATEAU MABINGWA WAPYA NIGERIA, OKPOTU MFUNGAJI BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top