• HABARI MPYA

  Thursday, September 14, 2017

  MANJI AACHIWA HURU BAADA YA KUFUTIWA MASHITAKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuachia huru Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji kwenye kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati akionyesha kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Manji na wenzake.
  Takribani miezi miwili imepita tangu Yusuf Manji na wenzake kusota rumande wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
  Mbali na Manji, wengine walioachiwa huru ni Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Quality Group Ltd, Deogratius Kisinda, Mtunza Stoo, Abdallah Sangey na Thobias Fwere.
  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa wameomba 'remove order' na kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri wanaiarifu Mahakama kwamba hakusudii kuendelea kuwashtaki Manji na wenzake katika kesi hiyo.
  Hivyo wanaomba kuiondoa kesi hiyo chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  Baada ya kueleza hayo Wakili wa Manji, Hajra Mungula ameeleza kuwa sheria inaruhusu DPP kufanya hivyo na kutokana na hatua hiyo, Hakimu Shaidi amesema kesi hiyo imefutwa na kuanzia sasa washtakiwa wapo huru.
  "Nendeni nyumbani hamkamatwi, hakuna kesi mpo huru," amesema DPP.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANJI AACHIWA HURU BAADA YA KUFUTIWA MASHITAKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top