• HABARI MPYA

  Monday, September 04, 2017

  LUKAKU AIPELEKA UBELGIJI KOMBE LA DUNIA URUSI 2018

  Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Ubelgiji dakika ya 75 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Ugiriki jana kwenye mchezo wa Kundi H kufuzu Kombe la Dunia mwakani Urusi uliofanyika Uwanja wa Georgios Karaiskaki mjini Pireas. Jan Vertonghen alianza kuifungia Ubelgiji ya kocha Roberto Martinez dakika ya 70, kabla ya  Zeca kuisawazishia Ugiriki. Ubelgiji sasa inafikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi nane na kuwa timu ya kwanza kufuzu fainali za mwakani za Kombe la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AIPELEKA UBELGIJI KOMBE LA DUNIA URUSI 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top