• HABARI MPYA

    Tuesday, September 12, 2017

    KAMUKOSO AREJEA KUWAVAA MAJI MAJI...CHIRWA NAYE YUKO ‘FULL’

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa Yanga, Thabani Scara Kamusoko leo ameanza mazoezi na timu yake, Yanga SC baada ya kuumia Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Njombe Mji.
    Kamusoko alitoka uwanjani anachechemea baada ya kuumia nyonga Jumapili na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mpya, Raphael Daudi dakika ya 49 siku hiyo Yanga ikishinda 1-0 ugenini.
    Lakini baada ya mapumziko ya siku moja ya jana, leo rasta huyo Mzimbabwe amefanya mazoezi na wenzake Uwanja wa kiwanda cha Chai Njombe kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Maji Maji Jumamosi Songea.
    Thabani Kamusoko (kulia) leo ameanza mazoezi Yanga SC baada ya kuumia Jumapili katika mchezo dhidi Njombe Mji

    Na katika mazoezi hayo, mchezaji huyo wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe alionekana amepona kabisa na kucheza kwa uchangamfu.
    Pamoja na Kamusoko, mchezaji mwingine wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe, Mzambia Obrey Chirwa naye amefanya mazoezi kikamilifu leo.   
    Kwa mara ya kwanza msimu huu, Chirwa alitokea benchi kipindi cha pili kwenda kumpokea Donald Ngoma Jumamosi katika mchezo wa ugenini pia dhidi ya Njombe Mji bao la Ibrahim Hajib likiipa Yanga ushindi wa 1-0.
    Baada ya hapo, mchezaji aliyeumia Julai mwaka huu jana na leo amefanya mazoezi kikamilifu kuelekea mechi na Maji Maji.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMUKOSO AREJEA KUWAVAA MAJI MAJI...CHIRWA NAYE YUKO ‘FULL’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top