• HABARI MPYA

    Thursday, September 07, 2017

    FIFA YAAMURU MCHEZO WA BAFANA NA SENEGAL URUDIWE

    IDARA ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), imeagiza marudio ya mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal uliofanyika Novemba 12, mwaka 2016. 
    Bafana Bafana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi y Simba wa Teranga Novemba mwaka jana, lakini ikabainika walimtumia refa kupanga ushindi huo.
    Uamuzi huo unafuatia uthibitisho wa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kuafiki kifungo cha maisha cha refa Joseph Lamptey wa Ghana kwa kuvurunda kimaamuzi katika mchezo huo, hivyo kuadhibiwa na Kamati ya Nidhamu ya FIFA kabla ya kukata Rufaa iliyodunda Kamati ya Rufaa. 
    Sadio Mane wa Senegal akimiliki mpra mbele ya mchezaji wa Afrika Kusini
    Mchezo huo utarudiwa Novemba mwaka 2017 katika kalenda ya kimataifa, katika tarehe ambayo itatajwa baadaye na wahuiska, Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
    Kama zzinavyosema Kanuni za Kombe la Dunia za FIFA, uamuzi huu unatakiwa kutekelezwa mara moja, lakini utahitaji uthibitisho wa Kamati ya Mashindano ya FIFA katika kikao chake kijacho Septemba 14.
    Bafana Bafana na Simba wa Teranga wote wapo Kundi D katika mchujo wa mwisho wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi, ingawa wapo mkiani nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde zilizofungana kwa pointi sita kila moja. Senegal ina pointi tano na Afrika Kusini ia pointi moja kuelekea mechi mbili za mwisho.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FIFA YAAMURU MCHEZO WA BAFANA NA SENEGAL URUDIWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top