• HABARI MPYA

    Friday, September 22, 2017

    FIFA KUTOA DOLA 333,000 CHALLENGE YA WANAWAKE RWANDA

    Na Canisius Kagabo, KIGALI
    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) litaipa Rwanda kiasi cha dola za Kimarekani 333,000 kwa ajili ya kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, inayotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Rwanda. 
    Akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali leo mjini Kigali, Rwanda, Mkuu wa Maendeleo ya Soka ya Wanawake Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), Rwamalika Felecite amethibitisha kwamba FIFA itatoa mchango kwa ajili ya mashindano hayo.
    “CECAFA wametuomba kuwa wenyeji wa kombe la CECAFA kwa wanawake, na fedha za kujitayarisha zitatoka FIFA, sisi tunapaswa kuwa wenyeji tu. Ni dola 333,000 FIFA, ili tuweze kutayarisha michezo hiyo. Tunapaswa kuwa na miundombinu mizuri kama viwanja, hoteli na kadhalika,” amesema Felecite.
    Baada ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiomba Rwanda kuwa mwenyeji michuano hiyo iliyopangwa kuanza Novemba 3 hadi 11, mwaka huu, imeelezwa fedha hizo ambazo ni zaidi ya Sh. Milioni 278 za Rwanda zinahitajika kukamilisha michuano hiyo.
    Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Fatma Samba Diouf Samoura alipokuwa nchini Rwanda alisema kwamba FIFA itasaidia nchi hiyo kwa kutoa fedha za kutayarisha mashindano ya CECAFA ya wanawake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FIFA KUTOA DOLA 333,000 CHALLENGE YA WANAWAKE RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top