• HABARI MPYA

    Tuesday, September 05, 2017

    CAMEROON YA KWANZA KUAGA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018 URUSI

    MABINGWA wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Cameroon hawatakuwepo kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kutolewa katika hatua ya mwisho ya mchujo jana.
    Kikosi cha Hugo Broos kilihitaji ushindi mbele ya Nigeria nyumbani, lakini kikaambuloia sare ya 1-1 na sasa hawatakuwemo kwenye Kombe la Dunia 2018, wakiwa timu ya kwanza ya Afrika kutolewa kutolewa katika hatua ya mwisho ya mchujo.
    Sare hiyo inakuja siku tatu baada ya Cameroon, timu ya kwanza ya Afrika kufika Robo Fainali ya Kombe la Dunia kufungwa 4-0 na Nigeria kwenye mchezo wa kwanza ugenini.
    Cameroon hawatakuwepo kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi  

    Katika mchezo wa jana, Nigeria walianza kupata bao mjini Yaounde lililofungwa na Moses Simon dakika ya 30 kabla ya mfungaji wa bao la ushindi la Cameroon kwenye fainali ya AFCON, Vincent Aboubakar kuisawazishia timunyae kwa penalti dakiak ya 75 jana.
    Timu tano zitakazomaliza kileleni mwa makundi yake zitafuzu moja kwa moja fainali za Kombe la Dunia mwakani na kwa sasa Tunisia, Nigeria, Ivory Coast, Burkina Faso na Uganda zinaongoza makundi yake na iwapo matokeo yatabaki hivyo kutakuwa na timu mbili kutoka Afrika kwenye kombe la Dunia mwakni, ambazo ni Burkina Faso na Uganda.
    Cameroon, washindi wa mataji matano ya AFCON – wamecheza fainali tano za Kombe la Dunia katika miaka ya 1982, 1990, 1994, 1998, 2002, 2010 na 2014 na mara moja ilifika Robo Fainali, mwaka 1990, ikitolewa na England katika muda wa nyongeza.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAMEROON YA KWANZA KUAGA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018 URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top