• HABARI MPYA

    Wednesday, September 06, 2017

    BEN POL ATOA ALBAMU MPYA KALI INA NYIMBO 15

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol '  maarufu kama kidume ameamua kuachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo The Best Ben Pol' itakayoanza kuwa mtaani Septemba 8, mwaka huu ikiwa ni siku yake maalum ya kuzaliwa.
    Mkali wa RnB Septemba 8 atasheherekea siku yake ya kuzaliwa huku akichia albamu hiyo, ambayo itakuwa ikimfikisha miaka 8 katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini. 
    Akizungumzia ujio wa albamu hiyo pamoja na wimbo wake mpya unaitwa 'Kidume' ambao amemshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Chidinma, alisema kuwa uwamuzi wake wa kutoa albamu ni kutaka kuendelea kuwa karibu na mashabiki wake ambao bila ya wao asikufika alipo.
    Ben Pol ameaachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo The Best Ben Pol' itakayoingia sokoni Septemba 8

    Pol alisema albamu mpya inatolewa rasmi kesho ambayo ni siku yake ya kuzaliwa itakuwa na  nyimbo 15, ikiwa na mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya kwa kushirikiana na wasanii wenzake wa muziki huo.
    Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu sasa ni mwaka wake wa nane katika safari yake ya muziki ikiwa ni pamoja na kuungana na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimuunga mkono kila anapotoa nyimbo zake mpya.
    Pol alisema ametoa albamu hiyo yenye mchanganyiko wa nyimbo zake mbalimbali ambazo amezifanya na kuweza kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
    Alisema kuwa katika albamu hiyo kuna nyimbo mbalimbali huku ya hizo ni pamoja na  Kidume, Tatu na Tuliza Boli, ambazo amewashirikisha Darasa na Rama Dee.
    Pol alisema katika kuhakikisha mashabiki wake wanapata vitu vizuri amefanya kazi nzuri kama kama katika nyimbo zake zilizopita ambazo mpaya leo zionaendelea kufanya vizuri.
    Baadhi ya nyimbo hizo ni Nikikupata, Maneno,Jikubali, Yatakwisha, Sophia, Moyo 
    Mashine, Pete na Phone. 
    "Mimi kama msanii nguli  hapa nchini na Afrika Mashariki niliyefanya kazi yangu kwa miaka minane sasa, naona si vibaya kuendeleza muziki wangu kwa kutoa zawadi kwa mashabiki wangu kwa kutoa albamu yangu  ya “Best of Ben Pol” ikiwa na nyimbo 15 nilizoshikirisha wasanii mbalimbali wkiwemo Darasa na Rama Dee” alisema Ben Pol.
    Alisema kama msanii   mwenye uwezo katika ukanda wa Afrika Mashariki ana amini kila mshabiki atapenda kupata albamu yake hiyo ambayo itakuwa katika mwezi wa Septemba ambao ni muhimu sana kwake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEN POL ATOA ALBAMU MPYA KALI INA NYIMBO 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top