• HABARI MPYA

    Sunday, August 13, 2017

    SIMBA YATUMIA BILIONI 1.3 KUSAJILI, KILOMONI ASIMAMISHWA...KAPUYA, MGOYI WAINGIZWA BARAZA LA WADHAMINI

    Na Abdallah Mshamu, DAR ES SALAAM
    JUMLA ya Sh. Bilioni 1.3 zimetumika kwa ajili ya usajili wa kikosi cha Simba SC msimu huu.
    Hayo yamesemwa na Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’ katika Mkutano wa kawaida wa kila mwaka uliofanyika kuanzia asubuhi ya leo kwenye Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (MNICC), Dar es Salaam.
    Abdallah amesema kwamba wamesajili kikosi madhubuti kwa gharama kubwa, lengo kubwa likiwa ni kurejesha heshima ya klabu yao na kwamba wachezaji wa kigeni pekee wamegharimu Sh. Milioni 679, zikiwemo Sh. Milioni 226 zilizotumika katika dirisha dogo Desemba mwaka jana.
    “Usajili wetu Simba mwaka huu umegharimu shilingi 1,359,500,000 kati ya hizo shilingi 679,500,000 zimetumika kwa usajili wa wachezaji wa kigeni pekee, zikiwemo shilingi  226,500,000 zilizotumika katika dirisha dogo,”amesema Abdallah.
    John Raphael Bocco ni moja wachezaji wapya walioigharimu Simba jumla ya Sh. Bilioni 1.3

    Kaimu huyo Mwenyekiti amesema kwamba mwaka huu klabu imetenga bajeti ya Sh. Billioni 4,7 na hadi sasa wana uhakika wa kupata Sh. Bilioni 3.3 tu kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya mapato.
    “Mwaka huu klabu hiyo mwaka imetenga bajeti ya shilingi 4,738,673,000, kiasi ambacho tutakusanya kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato ni Sh. bilioni 3,308,215,000, hivyo basi katika bajeti yetu kuna mapungufu wa shilingi 1,430,658,000 ambazo ukijumlisha na fedha za kutengeneza Uwanja wa Bunju utakaogharimu shilingi milioni 200,” amesema Abdallah.                        
    Katika hatua nyingine, Simba imemsimamisha uanachama mchezaji na kiongozi wake wa zamani, Mzee Hamisi Kilomoni ambaye pia ni Mwenyekiti a Baraza la Wadhamini.
    Salim Abdallah alipendekza mbele ya wanachama 927 Kilomoni aondolewe katika Baraza la Wadhamini kwa kitendo chake cha kufungua kesi Mahakama ya Kisuru wiki hii kupiga mkutano wa leo.
    Simba imemsimamisha uanachama Mzee Hamisi Kilomoni ambaye pia ni Mwenyekiti a Baraza la Wadhamini

    “Mzee Kilomoni amevunja Katiba ya Simba Ibara ya 18 kifungu cha 15 (b) ambayo haitaki kupeleka mambo ya soka mahakamani, ikiwa wana chombo cha kusimamia matatizo,”alisema Abdallah na wanachama wengi wakanyoosha mikono kukubali Kilomkoni aondolewe, huku wachache mno wakipinga. Sasa pigwe, wanachama kura ya mikono, wachache walipinga.
    Kilomini ametakiwa kuandika barua ya utetezi na kufuta kesi alitofungua Kisutu, tofauti na hivyo atafutwa kabisa uanachama.
    Katika hatua nyingine, Mkutano huyo umepitisha Waziri wa zamani wa Michezo, Profesa Juma Athumani Kapuya ameteuliwa kuziba pengo la Ally Sykes katika Baraza la Wadhamini, huku Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaj Adam Mgoyi akiteuliwa kuziba nafasi ya Kilomoni.                        
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YATUMIA BILIONI 1.3 KUSAJILI, KILOMONI ASIMAMISHWA...KAPUYA, MGOYI WAINGIZWA BARAZA LA WADHAMINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top