• HABARI MPYA

    Saturday, August 19, 2017

    SAID NDEMLA KWENDA SWEDEN WIKI IJAYO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa Simba Said Hamisi Ndemla anatarajiwa kuondoka wakati wowote kuanzia Jumatano ijayo, kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden, wakala wake amethibitisha hilo.
    Safari ya kiungo huo ilianza kusikika tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, ambapo sasa mambo yanaonekana kuiva na kuelekea nchini humo kwenye klabu ya AFC.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online, wakala wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo, amesema kwamba safari ya mchezaji imeiva na kuwa hati yake ya kusafiria itarajiwa kuwa tayari Jumanne na kuanzia Jumatano anaweza kuanza safari.
    Said Ndemla anatarajiwa kwenda Sweden wiki ijayo kwa mipango ya kucheza soka ya kulipwa 

    “Visa yake mchezaji huyo ilichelewa kidogo kutokana na taratibu za ubalozi lakini kwa sasa uhakika wa kupatikana Jumanne upon a hivyo kuanzia siku yoyote anaweza kwenye kufanya majaribio,” alisema Kisongo ambaye pia ni wakala wa mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta.
    Ndemla alitakiwa kwenda kufanya majaribio AFC ya Sweden ambayo anaichezea pia mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, lakini alishindwa kuondoka kutokana na klabu yake ya Simba kumuhitaji katika mechi za mwishoni mwa Ligi Kuu.
    Iwapo Ndemla akifuzu katika majaribio hayo na kuuzwa kwenye klabu hiyo, atakuwa mchezaji ni wa pili kuondoka katika klabu ya Simba kwa sasa baada ya hivi karibuni beki wa timu hiyo, Abdi Banda alitimkia Afrika Kusini kwenye klabu ya Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo.
    Banda aliondoka baada ya kumaliza mkataba wake na Simba na kukataa kuongeza mkataba mpya na kuamua kutimkia nchini humo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAID NDEMLA KWENDA SWEDEN WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top