• HABARI MPYA

    Friday, August 18, 2017

    RWANDA YAPATA PIGO KUELEKEA MECHI NA UGANDA KUFUZU CHAN

    RWANDA imepata pigo kubwa kuelekea mchezo wa marudiano Raundi ya Pili ya mchuno wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Kenya mwaka 2018 dhidi ya Uganda, kufuatia kuumia kwa mshambuliaji wake, Ernest Sugira.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye hivi karibuni amesaini mkataba wa mwaka mmoja na vigogo, APR baada ya kushindwa kufanhya vizuri AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alivunjika eneo la ugoko wakati wa mazoezi Jumanne ya Agosti 15, mwaka huu na anatakiwa kuwa nje kwa angalau miezi sita.
    Ernest Sugira amevunjika eneo la ugoko mazoezini Jumanne na anatakiwa kuwa nje ya Uwanja kwa miezi sita

    “Sugira amechanika ugoko wa mguu ake kushoto na atakuwa nje kwa miezi mitano hadi sita. Ni maumibu mabaya,” amesema Daktari wa timu ya Rwanda, Patrick Rutamu alipozungumza na Waandishi wa Habari mjini Kigali.
    Kocha wa Amavubi, Antoine Hey alimtegemea sana mshambuliaji huyo aliyerejea nyumbani kumsaidia kupindua matokeo ya kipigo cha 3-0 walichokipata kwenye mchezo wa kwanza watakapokuwa wanarudiana na The Cranes kesho mjini Kigali. 
    Amavubi wanatakiwa kushinda angalau mabao manne dhidi ya jirani zao, jambo ambalo Hey amesema litakuwa sawa na kupanda mlima mkubwa.
    Licha ya pigo la Sugira, beki mkongwe, Aimable Rucogoza na mshambuliaji Bernabe Mubumbiyi pia wataukosa mchezo huo wa kufuzu CHAN kwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati kutokana na kuwa kwenye kifungo cha adhabu za kadi za njano.
    Pamoja na hayo, habari njema kwa Hey ni kuwepo kwa kipa Eric Ndayishimiye, ambaye alikuwa anatumikia adhabu kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Kampala. Suluhisho lingine katika safu ya ushambuliaji ni Gilbert Mugisha, Innocent Nshuti na Christophe ‘Abeddy’ Biramahire.
    "Mchezo wa marudiano utakuwa tofautu. Tumefungwa 3-0 lakini tunaweza kufanya vizuri nyumbani kwetu. Siwezi kuwalaumu wachezaji wangu kwa sababu walijaribu kila kitu na wanjituma sana na wamejipanga sana," alisema Hey.
    Rwanda inawania kucheza Fainali za CHAN kwa mara ya tatu baada ya mwaka 2011 nchini Sudan na 2016 walipokuwa wenyeji na Fainali za mwakani zitaanza Januari 12 hadi Februari 4 mwaka 2018 nchini.

    RATIBA MECHI ZOTE ZA KUFUZU CHAN
    Kanda ya Kati
    19.08.2017 Kinshasa DRC vs Kongo (0-0)
    19.08.2017 Yaounde Cameroon vs Sao Tome (2-0)
    Kanda ya Mashariki na Kati
    19.08.2017 Kigali Rwanda vs Uganda (0-3)
    19.08.2017 El Obeid Sudan vs Ethiopia (1-1)
    Kanda ya Kaskazini
    18.08.2017 Sfax               Libya vs Algeria (2-1)
    18.08.2017 Rabat Morocco vs Misri (1-1)
    Kanda ya Kusini
    19.08.2017 Ndola Zambia vs Afrika Kusini (2-2)
    19.08.2017 Luanda Angola vs Madagascar (0-0)
    20.08.2017 Windhoek Namibia vs Comoro (1-2)
    kanda ya Magharibi A
    19.08.2017 Bamako Mali vs Mauritania (2-2)
    22.08.2017 Conakry         Guinea vs Senegal (1-3)
    Kanda ya Magharibi B
    20.08.2017 Kumasi Ghana vs Burkina Faso (2-2)
    19.08.2017 Kano Nigeria vs Benin (0-1)
    19.08.2017 Abidjan Ivory Coast vs Niger (1-2)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RWANDA YAPATA PIGO KUELEKEA MECHI NA UGANDA KUFUZU CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top