• HABARI MPYA

    Thursday, August 17, 2017

    KISA MISHAHARA MIWILI, BOSSOU AITISHIA KUIPELEKA YANGA FIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa zamani wa Yanga, Mtogo Vincent Bossou anataka kupeleka malalamiko Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) juu ya madai ya kutolipwa mishahara ya miezi miwili na klabu hiyo.
    Bossou ameondoka Yanga mwezi uliopita baada ya kumaliza mkataba wake, lakini amesema anadai mishahara ya miezi miwili na kama klabu hiyo itaendelea kupuuza madai yake, atapeleka kesi FIFA.
    Kupitia kwa wakala wake, Mganda Gibby Kalule, Bossou amesema kwamba viongozi wa Yanga, Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa na Mhasibu, Baraka Deusdedit wamekuwa wakipuuza jitihada zake za kudai malimbikizo yake hayo hata baada ya kuondoka, hivyo hataki kulaumiwa na mashabiki wa timu hiyo atakapokwenda FIFA.
    Vincent Bossou anataka kuipeleka Yanga FIFA kwa madai ya kutolipwa mishahara ya miezi miwili

    “Muda si mrefu nitawatumia Yanga barua mpya, lakini niwatake mashabiki wa Yanga kuzungumza na viongozi wao, kwani nimewatumia barua, sitaki kuingia katika matatizo na Yanga kwa kuwa Mkwasa aliniahidi lakini kwa sasa kila nikimtumia ujumbe lakini hajajibu.” Amesema Bossou.
    Amesema ametuma barua pepe kwa Mkwasa na Deusdedit, lakini wote wamepuuza, hivyo atakapochukua hatua kubwa zaidi asilaumiwe.
    “Nasubiri wanijibu barua yangu na kunilipa fedha zangu iwapo wakishindwa kufanya hivyo meneja wangu atachukua hatua zaidi,” alisema Bossou.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KISA MISHAHARA MIWILI, BOSSOU AITISHIA KUIPELEKA YANGA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top