• HABARI MPYA

    Tuesday, August 15, 2017

    KIBOKO YAIBEBA NDANDA FC, YAIPA UDHAMINI MWAKA MMOJA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya Motisun Group Limited kupitia Kiboko imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na klabu ya Ndanda FC ya Mtwara, inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Hiyo ikiwa ni siku chache lanka ya Ligi Kuu Bara ianze kutimua vumbi Agosti 26, mwaka.
    Akizungumza na jijini Dar, Mshauri wa Masoko na Biashara wa Ndanda, Peter Simon alisema wanaushukuru udhamini huo ambao utawasaidia wao kupambana na mikikimikiki ya ligi kuu kwenye msimu ujao ambao anaamini utakuwepo mkubwa. 
    Simon alisema, udhamini utawawezesha wao timu yao kusafiri nje ya mikoa kwa ajili mechi za ugenini huku wakiahidi kutowaangusha kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja. 
    "Niwaahidi Motisun Group kupitia kwa bidhaa yao ya Kiboko kuwatangaza vema kupitia timu yao itakayoshiriki ligi kuu. 
    "Ndanda tunaamini kuwa kupitia timu yetu wataongeza idadi ya wateja kutokana kuwatangaza vema, "alisema Simon. 
    Kwa upande wa Motisun kupitia kwa Mkuu wa Masoko, Edward Mlyansi alisema kuwa "Kwa kuanza wanaanza na udhamini huo wa mwaka mmoja na baadaye watauboresha zaidi hapo baadaye.
    "Kikubwa wanataka kuona timu ikipata matokeo mazuri na kuleta ushindani mkubwa na hatutaki kuona migogoro katika timu, "alisema Mlyansi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIBOKO YAIBEBA NDANDA FC, YAIPA UDHAMINI MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top