• HABARI MPYA

  Tuesday, July 11, 2017

  YANGA YAMSAJILI KIPA WA SERENGETI BOYS ALIYEITWA STARS

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imekamilisha idadi ya makipa watatu baada ya kumsaini na kipa wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Ramadhani Awam Kabwili.
  Mlinda mlango huyo atakayetimiza umri wa miaka 17 Desemba 11, mwaka huu alidaka mechi zote za Serengeti Boys kwenye Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon na kusifiwa mno kwa kiwango kizuri alichoonyesha.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wamesajili Kabwili baada ya kuachana na makipa wao wawili wa muda mrefu, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ waliomaliza mikataba yao.
  Ramadhani Awam Kabwili amesajiliwa Yanga SC baada ya kufanya vizuri na Serengeti Boys

  Hafidh amesema Kabwili anaungana na kipa mwingine mpya, Mcameroon Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon na Benno Kakolanya ambaye anakwenda kwenye msimu wa pili tangu asajiliwe kutoka Prisons ya Mbeya.
  Yanga SC, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wameanza mazoezi leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya, ingawa hawakuwa na kipa mmoja baada ya 
  Rostand na Kakolanya kutotokea, wakati Kabwili yuko na timu ya taifa ya wakubwa, Taifa Stars mjini Mwanza.  
  Kabwili ameitwa kwa mara ya kwanza Taifa Stars, ambayo Jumamosi itamenyana na Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAMSAJILI KIPA WA SERENGETI BOYS ALIYEITWA STARS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top