• HABARI MPYA

    Saturday, July 08, 2017

    VYETI VYAWAPONZA ‘JULIO’ NA MALIMA ‘JEMBE ULAYA’ KUENGULIWA UCHAGUZI TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemuengua kocha maarufu nchini, Jamhuri Mussa ‘Julio’ Kihwelo kuwania uongozi wa shirikisho hilo kwa sababu hakuwasilisha vyetu vya elimu ya sekondari. 
    Sababu kama hizo zinazomuondoa beki huyo wa zamani wa Simba kwenye kuwania uongozi wa TFF, ndizo pia zimemfanya beki wa zamani wa Yanga, Bakari Juma Malima ‘Jembe Ulaya’ naye kuenguliwa kwenye kinyng’anyiro hicho na wote walikuwa wanawania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda Maalum Dar es Salaam.
    Pamoja na hayo, Kamati hiyo imeyapeleka majina ya wagombea iliyowapitisha kuwania uongozi wa shirikisho hilo Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) kwa ukaguzi wa vyeti vyao vya elimu kabla ya kupitishwa rasmi kwa uchaguzi wa Agosti 12 mjini Dodoma.
    Jamhuri ‘Julio’ Kihwelo ameenguliwa kwenye uchaguzi wa TFF kwa kushindwa kuwasilisha vyetu vya elimu ya sekondari 

    Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Mohammed Mchengerwa amesema leo katika taarifa yake kwamba baada kumaliza kikao chao kilichoanza asubuhi ya leo, wanayapeleka majina yaliyopitishwa kwa ukaguzi wa elimu zao, utakaofanywa na wizara ya Elimu.
    “Wale ambao hawakupata nafasi wanayohaki ya kukata Rufaa, hali kadhalika Majina yaliyopitishwa sasa yanapelekwa kwa ukaguzi wa Elimu yao unaofanywa na wizara ya Elimu,”amesema.
    Amesema katika majina ya sasa, wapo waliokatwa awali ambao wamerejeshwa na wapo waliopitishwa awali, ambao sasa wameondolewa kutokana na vigezo kutofuatwa na kanuni.
    Waliopitishwa ni Ally Mayay, Athumani Nyamlani, Frederick Mwakalebela, Imani Madega, Wallace Karia, Shija Richard na Emmanuel Kimbe kwa nafasi ya Urais, Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa kwa nafasi ya Umakamu wa Rais.
    Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka Kanda namba 1, Mikoa ya Kagera na Geita; Salum Chama, Kaliro Samson na Leopold 'Taso' Mukebezi, Kanda namba 2 Mikoa ya Mara na Mwanza; Vedastus Lufano, Ephraim Majige, Samuel Daniel na Aaron Nyanda na Kanda namba 3 mikoa ya Shinyanga na Simiyu; Benista Rugora, Mbasha Matutu na Stanslaus Nyongo.
    Kanda namba 4 mikoa ya Arusha na Manyara; Omari Walii, Sarah Chao na Peter Temu, Kanda namba 5 mikoa ya Kigoma na Tabora; John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael, Kanda namba 6 mikoa ya Katavi na Rukwa; Kenneth Pesambili na Baraka Mazengo.
    Kanda namba 7 mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa; Elias Mwanjala, Cyprian Kuyava, Erick Ambakisye na Abousuphyan Silliah, Kanda namba 8 mikoa ya Njombe na Ruvuma; James Mhagama, Golden Sanga, Vicent Majili na Yono Kevela na Kanda namba 9 mikoa ya Lindi na Mtwara; Athuman Kambi na Dunstan Mkundi.
    Kanda namba 10 mikoa ya Dodoma na Singida ni Hussein Mwamba, Mohamed Aden, Stewart Masima, Ally Suru na George Benedict, Kanda namba 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro ni Charles Mwakambaya, Gabriel Makwawe na Francis Ndulane. 
    Kanda namba 12 mikoa ya Kilimanjaro na Tanga; Khalid Mohamed na Goodluck Moshi, Kanda namba 13 mkoa wa Dar es Salaam; Emmanuel Ashery, Ayoub Nyenzi, Shaffih Dauda, Abdul Sauko, Peter Mhinzi, Ally Kamtande, Said Tully, Mussa Kisoky, Lameck Nyambaya, Ramadhani Nassib, Aziz Khalfan, Saad Kawemba na Bakari Malima.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VYETI VYAWAPONZA ‘JULIO’ NA MALIMA ‘JEMBE ULAYA’ KUENGULIWA UCHAGUZI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top