• HABARI MPYA

    Friday, July 07, 2017

    SUDAN YAENGULIWA MICHUANO YA AFRIKA KWA KUFUNGIWA FIFA

    KLABU za Sudan zinazoshiriki michuano ya Afrika zimeondolewa kufuatia nchi yao kusimamishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
    FIFA imelifungia Shirikisho la Soka Sudan (SFA) katika barua yake ya Julai 6 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Fatma Samoura.
    Kwa mujibu wa ibara ya 13 ya Katiba ya FIFA, SFA inapoteza haki zote za uanachama, na uwakilishi wa timu zake za taifa na klabu nao unafutwa pia.
    Na kutokana na maamuzi hayo, klabu tatu za Sudan, El Hilal, El Merreikh zilizokuwa kwenye Ligi ya Mabingwa na Al Hilal Obeid iliyokuwa Kombe la Shirikisho zote zimeondolewa kwenye michuano hiyo.
    Waziri wa Sheria wa Sudan aliagiza Rais wa SFA, Mutasim Gaafar Sir Elkhatim aondolewe Juni 2‚ na nafasi yake kuchukuliwa na Abdel Rahman Sir Elkatim jambo ambalo ni kinyume cha maelekezo ya FIFA, inayozuia Serikali kuingilia michezo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUDAN YAENGULIWA MICHUANO YA AFRIKA KWA KUFUNGIWA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top