• HABARI MPYA

  Wednesday, July 05, 2017

  SINGIDA UNITED NAYO YAIBOMOA SIMBA, YAMCHUKUA PASTORY ATHANAS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAGENI wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Singida United wameendelea kujiimarisha kwa changamoto mpya baada ya leo kumsaini mshambuliaji Pastory Athanas kutoka Simba SC.
  Athanas anaondoka Simba SC baada ya miezi sita tu, tangu asajiliwe kutoka Stand United ya Shinyanga, jambo ambalo halikutarajiwa hususan baada ya kuonyesha kipaji kizuri tu Msimbazi.  
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Athanas amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu hiyo.
  Mshambuliaji Pastory Athanas akiwa ameshika jezi ya Singida Unted baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kutoka Simba SC
  Na amesema usajili huo ni pendekezo la kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm ambaye ni shabiki wa mchezaji huyo tangu akiwa Stand.
  “Kocha Pluijm wakati Yanga alikuwa anapenda sana Athanas alipokuwa Stand, bahati mbaya hakuwa kumsaini pale Yanga, lakini baada ya kuja huku kwetu, ametimiza ndoto za kufanya kazi na kijana huyo,”amesema Sanga. 
  Sanga ni mchezaji wa pili kwa siku hii moja ya leo kuwapa mkono wa kwaheri Wekundu wa Msimbazi, baada ya Ibrahim Hajib kusaini pia mkataba wa miaka miwili na mahasimu, Yanga SC.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED NAYO YAIBOMOA SIMBA, YAMCHUKUA PASTORY ATHANAS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top