• HABARI MPYA

  Wednesday, July 05, 2017

  SIMBA YAMUONDOA KOCHA MKENYA, ‘SHILTON’ ACHUKUA NAFASI KUWANOA MAKIPA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA imeachana na kocha wake wa makipa, Mkenya, Iddi Salim na kumchukua kipa wake wa zamani, Muharami Mohammed ‘Shilton’.
  Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba Muharami, aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys amefikia makubaliano na klabu kwa kazi hiyo.
  Na kwa sababu hiyo, wazi Simba inachana na Mkenya Salim aliyekuwa anafanya kazi Msimbazi kwa mara ya pili, baada ya awali miaka miwili iliyopita kuwa chini ya Muingereza, Dylan Kerr.
  Muharami Mohammed ‘Shilton’ ndiye kocha mpya wa makipa Simba SC

  Na hakuna kingine ambacho kinaifanya Simba ibadilishe kocha wa makipa, zaidi ya kuteteraka kwa kwa viwango vya udakaji wa makipa msimu uliopita.
  Simba imemsajili kipa wa Azam FC, Aishi Manula na inasemekana ina mpango wa kuachana na kipa wake namba moja, Daniel Agyei baada ya miezi sita tangu imsaili kutoka Medeama SC ya kwao, Ghana akiwa katika kiwango cha juu. 
  Imemsajili pia aliyekuwa kipa wa akiba wa Mbaao FC, Emmanuel Mseja na inasemekana inataka kumuacha kipa wa pili, Peter Manyika, naye sababu ya kushuka kiwango.
  Kwa ujumla ubora wa makipa wa Simba umekuwa si wa uhakika tangu kuondoka kwa Iddi Pazi ‘Father’ aliyekuwa kocha wa makipa wa timu hiyo.
  Inaaminika Pazi, kipa wa zamani wa kihistoria Simba SC ni miongoni mwa maakocha watatu bora wa makipa, pamoja na Juma Pondamali wa Yanga na Manyika Peter ambaye kwa sasa hana timu baada ya kufanya kazi hiyo timu ya taifa, Taifa Stars. 
  Muharami alikuwa kipa wa Simba SC mwaka 1999 na 2000 kablaa ya kwenda Msumbiji ambako alicheza kwa muda mrefu wa maisha yake hadi kustaafu miaka mitano iliyopita na kuwa kocha.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMUONDOA KOCHA MKENYA, ‘SHILTON’ ACHUKUA NAFASI KUWANOA MAKIPA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top