• HABARI MPYA

    Thursday, July 06, 2017

    SAMATTA APEWA JEZI NAMBA 10 GENK

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta kuanzia msimu ujao atakuwa anavaa jezi namba 10 badala ya 77 katika klabu yake, KRC Genk ya Ubelgiji.
    Kupitia akaunti yake ya Instagram, Genk imeandika; “Mbwana Samatta msimu ujao atachezea (jezi) namba 10,”.
    Na hiyo ndiyo jezi ambayo Samatta anaivaa hadi katika timu yake ya taifa, Taifa Stars ambayo yeye ni Nahodha. 
    Lakini aliposajiliwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), klabu yake ya mwisho ya Afrika kuchezea, Samatta alianza kwa kuvaa jezi namba 15 kabla ya baadaye kupewa namba 9.
    Baada ya msimu mmoja na nusu, Samatta amecheza mechi 60 Genk na kufunga mabao 20 tangu amejiunga nayo Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC, kati ya hizo mechi 18 alicheza msimu uliopita na 42 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 38 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 28 msimu huu.
    Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao yake 20, 15 amefunga msimu huu na matano msimu uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA APEWA JEZI NAMBA 10 GENK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top