• HABARI MPYA

  Tuesday, July 11, 2017

  NIYONZIMA ATUA RAYON SPORTS KWA FARANGA MILIONI 7.5

  MWANASOKA wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima amekamilisha uhamisho wake kutoka Mukura Victory Sports kwenda kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda, Rayon Sports kwa dau la usajili la Faranga  Milioni 7.5.
  Niyonzima, ambaye amedumu kwa miaka miwili Mukura, amesaini mkataba wa miaka miwili—akiungana na wachezaji wengine watatu wapya akiwemo beki wa kushoto, Eric Rutanga kutoka APR FC kwa Faranga Milioni 6, kiungo Yussuf Habimana kutoka Mukura kwa Faranga Milioni 5.5, beki wa kulia Saddam Nyandwi kwa Faranga Milioni 5 kutoka Espoir.
  Ally Niyonzima amekamilisha uhamisho wake kutoka Mukura Victory Sports kwenda Rayon kwa dau la Faranga  Milioni 7.5.

  Usajili wa wanne hao umethibitishwa na Katibu Mkuu na Msemaji wa Rayon Sports, Olivier Gakwaya, aliyesema kwamba wamesaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja.
  Niyonzima bado amebakiza mkataba wa mwaka mmopja Mukura, maana yake klabu ya Huye itapata Faranga Milioni 2.5, wakati Rutanga, Habimana na Nyandwi wamesaini wakiwa wachezaji huru.
  Wakati huo huo: Gakwaya amesema kipa na Nahodha  wa timu hiyo, Eric ‘Bakame’ Ndayishimiye amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la Faranga Milioni 8 kubaki.
  Wachezaji wengine waliosaini mikataba mipya ni kiungo mshambuliaji Kevin Muhire, winga wa kulia, Nova Bayama na kiungo mkabaji, Olivier ‘Seif’ Niyonzima.
  Hata hivyo, mabingwa hao wa Ligi wamempoteza kocha wao, Djuma Masudi, aliyejiuzulu wiki iliyopita huku washambuliaji Dominique Savio Nshuti na Moustapha Nsengiyumva wakihamia AS Kigali na Polisi FC.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIYONZIMA ATUA RAYON SPORTS KWA FARANGA MILIONI 7.5 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top