• HABARI MPYA

    Thursday, July 06, 2017

    MWANAMUZIKI NGULI TANZANIA, SHAABAN DEDE AFARIKI DUNIA

    MWIMBAJI mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa. Dede, mwanamuziki wa Msondo ambaye pia aling’ara na bendi za Mlimani Park “Sikinde”, Bima Lee na OSS, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari pamoja na figo. 
    Saluti5 imemnukuu Hamad Dede, mtoto wa marehemu, akisema kwamba mpendwa wao huyo amewatoka. “Baada ya kama masaa mawili tutakaa kama familia na kutoa taarifa rasmi ya msiba utakuwa wapi na mazishi ni lini ingawa kuna kuna zaidi ya asilimia 70 kuwa tutazika kesho,” alisema Hamad. 
    Onyesho la mwisho Dede kushiriki ni lile lililofanyika Travertine Hotel, Magomeni la mpambano wa Msondo na Sikinde Mei 20 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANAMUZIKI NGULI TANZANIA, SHAABAN DEDE AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top