• HABARI MPYA

  Friday, July 07, 2017

  MTOTO WA RONALDO LIMA AITWA TIMU YA TAIFA BRAZIL U-18

  MTOTO wa kwanza wa mwanasoka bora wa zamani wa dunia, Ronaldo Lima alitwaye, Ronald Nazario de Lima amechukuliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil chini ya umri wa miaka 18 kwa ajili yaa Michezo ya Maccabiah mwaka huu.
  MIchezo ya Maccabiah ni ya tatu kwa ukubwa dunian, ambayo hushirikisha wanamichezo wasiopungua 10,000 kutoka mataifa 85, naa inaajulikana kama Olimpiki ya Kiyahudi

  Mtoto wa Ronaldo Lima, aitwaye Ronald (nyuma kulia) akiwa na kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 cha Brazil PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Na huu unaweza kuwa mwanzo wa kizazi kipya cha Ronaldo, kwa Mbrazil huyo kujaribu kuyafukuzia mafanikio ya Mreno, Cristiano.
  Ronald alizaliwa mjini Milan wakati baba yake anachezeaa klabu ya Inter Milan mwaka 1999. Na bahati nzuri kijana huyo wa umri wa miaka 17 soka amerithi kutoka kwa wazazi wake wote wawili, kwani hata mama yake, Milene Domingues alikuwa mchezaji wa kimataifa Brazil.
  Kwa pamoja wazazi wake wamecheza mechi 118 timu ya taifa na mechi 775 za klabu, maana yake huu ni ukoo kweli wa soka. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTOTO WA RONALDO LIMA AITWA TIMU YA TAIFA BRAZIL U-18 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top