• HABARI MPYA

  Monday, July 10, 2017

  MKHITARYAN 'ABAMBWA LIVE' NA MKE WA ZAMANI WA DJIBRIL CISSE

  NYOTA wa Manchester United, Henrik Mkhitaryan amepigwa picha akiwa na mke wa zamani wa Djibril Cisse, Jude Cisse 'wakila bata' pamoja San Carlo Chiccetti.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Armenia amesafiri kwenda Los Angeles na wachezaji wengine wa Manchester United jana jioni, lakini Alhamisi alikuwa Italia.
  Akapigwa picha akiwa na mtalaka huyo wa Cisse, Jude mwenye umri wa miaka 42 wakiwa wanazungumza kwa karibu mno.
  Jude aliolewa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Cisse kwa miaka saba kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2012 na na wamezaa watoto watatu kabla ya kutalikiana.
  Mwaka 2015 akaelezea maisha yake katika Channel 5 documentary kama mama anayelea watoto peke yake, jambo ambalo lilimvutia mumewe huyo wa zamani na akamjibu kaatika Twitter. Sasa Jude anaendesha biashara ya spa mjini Cheshire.

  Henrikh Mkhitaryan is photographed deep in conversation with Jude Cisse PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Na baada ya 'bata' hilo, Mkhitaryan sasa yupo Marekani na timu yake Manchester United wakijiandaa na msimu mpya.
  Kikosi cha Jose Mourinho kitacheza mechi ya kirafiki na LA Galaxy, Real Salt Lake City, Manchester City na Real Madrid kuanzia Julai 16.
  Na Mkhitaryan, mwenye umri wa miaka 28, anatakiwa kuwadhihirishia mashabiki juu ya uwezo wake, baada ya kumponda kutokana na picha aliyoposti kwenye mitandao ya kijamii akiwa na kitambi.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKHITARYAN 'ABAMBWA LIVE' NA MKE WA ZAMANI WA DJIBRIL CISSE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top