• HABARI MPYA

  Thursday, July 06, 2017

  MAN UNITED YAWAPIGA KUMBO CHELSEA USAJILI WA LUKAKU

  KLABU ya Manchester United iko tayari kuipiku Chelsea katika kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku kwa dau la Pauni Milioni 100.
  Inafahamika kocha Jose Mourinho yupo karibuni kukamilisha usajili huo wa dau la rekodi la dunia, kuvunja rekodi ya Paul Pogba aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 89 kurejea Old Trafford mwaka jana.
  Mshambuliaji wa Everton, Lukaku ambaye amefunga mabao 26 msimu uliopita, alitarajiwa kurejea Stamford Bridge, lakini mahusiano baina ya klabu hizo mbili yamevurugika tangu Chelsea ishindwe kumsajili John Stones mwaka 2015.  
  Siri; Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho akimnong'oneza Romelu Lukaku sikioni wakati walipokuwa pamoja Chelsea mwaka 2015 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Mourinho alikuwa kocha wa Chelsea, ambaye alimuuza Lukaku kwenda Goodison Park miaka mitatu iliyopita, lakini yuko tayari kufanya naye kazi tena nyota huyo Mbelgiji
  Huku Lukaku akitarajiwa kwenda Old Trafford, Everton inatumai nayo kumrejesha Wayne Rooney Uwanja wa Goodison kutoka United, ingawa klabu hizo bado hazijafikia makubalino.
  Rooney anakaribia kurejea Merseyside miaka 13 baada ya kuondoka kwenda Old Trafford kwa dau la Pauni Milioni 27, bada ya Everton kuoyesha nia ya kumsajili tena.
  Dhamira ya Everton kumsajili Rooney na United kumtaka Lukaku vinajenga uwezekano wa makubaliano na wachezaji hao wakabadilishana jezi msimu ujao. 
  Vipengele kadhaa vimejadiliwa, ikiwemo United kulipa miaka miwili iliyobaki kwenye mkataba wa Rooney na kumruhusu kuondoka kama mchezaji huru, na mkopo wa muda mrefu wa msimu, ambao utafanya klabu hizo mbili zichaangie kumlipa mshahara wake wa Pauni 230,000 kwa wiki.
  Wakala wa Rooney, Paul Stretford alikutana na Bill Kenwright katika ofisi za Mwenyekiti huyo wa Everton mjini London Jumatano na mazungumzo ya kina yalitarajiwa kuchukua nafasi.
  Wakati wote Everton limekuwa chaguo la Rooney kuliko kwenda China au America, na amethibitisha kwamba baada ya United kushinda fainali ya Europa League mwezi Mei hiyo ndiyo klabu pekee anaweza kuichezea baada ya kuodoka Old Trafford.
  Lakini hadi sasa, Everton ndiyo wanasuasua wakiwa wanataka kumsajili kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 10 na mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye kiwango chake kimeshuka.
  Walijaribu kupeleka ombi la kumsajili kwa mkopo Januari lakini wakakataliwa na wiki hii mpango umeibuka tena baada ya Rooney kuamua kubaki England baada ya kufurahia na familia yake Mykonos.
  Wanahisa wakuu wa Everton, Farhad Moshiri na Kenwright wanaona thamani ya klabu itapanda wakifanikiwa kumrejesha Rooney sehemu aliyoibukia kisoka na wanaa matumaini ya kumpata.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAWAPIGA KUMBO CHELSEA USAJILI WA LUKAKU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top