• HABARI MPYA

  Monday, July 10, 2017

  MAN UNITED WATAKA KUIPIGA BAO CHELSEA NA KWA BAKAYOKO PIA

  KLABU ya Manchester United inataka 'kuipiga bao' lingine Chelsea katika kuwania saini ya kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko.
  Timu hiyo ya Old Trafford imetoa ofa ya Pauni Milioni 40 kwa ajili ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa, hivyo sasa inaongoza mbio za kuwania saini ya Bakayoko, ambaye alikuwa kivutio kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
  Chelsea ilikuwa na matumaini ya kumnasa Bakayoko kabla ya mwishoni mwa wiki, licha ya kufanyiwa upasuaji wa goti ambao utamfanya akosekane mwanzoni mwa msimu.

  Manchester United inataka kuipiga bao Chelsea katika usajili wa Tiemoue Bakayoko pia PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Bakayoko, ambaye ameposti picha akiwa mbele ya ndege leo, mwezi uliopita alifanyiwa upasuaji wa goti ambalo lilikuwa linamsumbua kwa maumivu tangu Februari.
  Mpango wa kwenda kufanyiwa vipimo vya Chelsea mjini London umefutwa na klabu hizo mbili hazijafikia makubaliano ya ada ya uhamisho. 
  Na United sasa imeingilia kati mpango huo nayo inataka kumalizana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 haraka.
  Rasmi leo kocha Mreno, Jose Mourinho amefanikiwa kuipiku klabu yake ya zamani, Chelsea katika vita ya kuwania saini ya mshambuliaji Mbelgiji, Romelu Lukaku aliyesaini mkataba wa miaka Manchester United kutoka Everton kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 75.
  Dau hilo linamfanya Lukaku awe mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka ya Uingereza na mkataba wake wa miaka mitano una kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja zaidi. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WATAKA KUIPIGA BAO CHELSEA NA KWA BAKAYOKO PIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top