• HABARI MPYA

  Thursday, July 13, 2017

  MAN UNITED SASA KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI TENA

  Romelu Lukaku amejiunga na Manchester United hivi karibuni kutoka Everton PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  10 BORA YA KLABU TAJIRI DUNIANI KWA MUJIBU WA  FORBES

  1. Dallas Cowboys
  2. New York Yankees
  3. Manchester United
  4. Barcelona
  5. Real Madrid
  6. New England Patriots
  7. New York Knicks
  8. New York Giants
  =9. San Francisco 49ers
  =9. Los Angeles Lakers 
  TIMU ya Manchester United imezipindua Barcelona na Real Madrid na kupanda juu kwenye orodha ya klabu za soka tajiri duniani - na kushika nafasi ya tatu kwa michezo yote.
  Ni Dallas Cowboys pekee inayocheza NFL yenye thamani ya Pauni Bilioni 3.25 na New York Yankees inayocheza Ligi Kuu Baseball Marekani yenye thamani ya Pauni Bilioni 2.86 zinaizidi timu hiyo ya Ligi Kuu ya England kwa sasa.
  United ina thamani ya Pauni Bilioni 2.85, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11 kutoka Pauni Bilioni 2.57 mwaka 2016, licha ya kushindwa kutaji la Ligi Kuu ya England au Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mwaka 2013. 
  Wamepanda kutoka nafasi ya tano hadi ya tatu katika orodha ya 50 Bora za jarida la Forbes la Marekani. Wakati huo huo, wapinzani wao wakubwa, Liverpool ni kati ya timu mbili, pamoja na wakali wa NBA, Houston Rockets walioporomoka kwenye chati hiyo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED SASA KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI TENA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top