• HABARI MPYA

  Tuesday, July 11, 2017

  MAMA SAMIA KUMSABAHI ROONEY ALHAMISI KABLA YA MECHI NA GOR MAHIA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan atapata fursa ya kumsabahi mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney kabla ya timu yake mpya, Everton kumenyana na Gor Mahia Alhamisi mjini Dar es Salaam.
  Refa maarufu nchini, Israel Mujuni Nkongo ndiye atachezesha mchezo huo wa kirafiki kati ya Everton ya England na Gor Mahia ya Kenya Uwanja wa Taifa, Jijini.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Gulam Abbas amesema kwamba maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika na Everton wataingia nchini kesho asubuhi.
  Everton wanatarajiwa kuja na Wayne Rooney na watavaa jezi hizi za ugenini keshokutwa

  “Everton wanaingia kesho majira ya asubuhi na Alhamisi watacheza mchezo wa kirafiki na timu kutoka nchini Kenya, Gor Mahia,”amesema Mwenyekiti huyo wa zamani wa klabu ya Yanga.
  Aidha, Mkurugenzi huyo Mkuu wa zamani wa Bodi ya Michezio ya Kubahatsha nchini amesema kwamba mgeni rasmi katika mchezo huo wa kihistoria atakuwa ni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
  Gor Mahia ilipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup, ikiwafunga mahasimu, AFC Leopatrds 3-0
  Kikosi cha kocha Ronald Koeman kinatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kesho asubuhi kikiwa na mshambuliaji wake mpya, Wayne Rooney atakayevaa jezi namba 10 iliyoachwa wazi na Romelu Lukaku aliyehamia Manchester United kwa dau la Pauni Milioni 75.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anarejea Everton miaka 13 baada ya kuondoka kuhamia United akiwa kinda wa umri wa miaka 18 tu mwaka 2004.
  Na siku mbili tu baada ya kusaini kurejea The Toffees, Nahodha wa zamani wa Man United naq England amethibitisha kuja Afruika katikati ya wiki.
  “Naangalia mbele kwa hilo – itakuwa safari nzuri, itakuwa nzuri na ninatumaini nitaingia uwanjani na kupata muda Fulani wa kucheza. Ni vizuri unaposafiri ugenini na timu. Ni vizuri kuwa kwenye hoteli na wachezaji, kutumia muda zaidi na wao na kuwafahamu zaidi,” alisema Rooney jana.
  “Sijawahi kufika Tanzania kabla, hivyo ninaangalia mbele kwa hilo,”amesema
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMA SAMIA KUMSABAHI ROONEY ALHAMISI KABLA YA MECHI NA GOR MAHIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top